(ABNA24.com) Sayyid Abbas Mousavi, amesema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari wa ndani na wa nje ambapo amebainisha kwamba, uhusiano wa kirafiki wa Iran na nchi za eneo hususan nchi rafiki upo palepale na kwamba, hakuna wakati ambao uhusiano wa Tehran na Uturuki ulikuwa mzuri kama ilivyo hivi sasa, lakini hii haina maana ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kulegeza kamba kuhusiana na misimamo yake ya kimsingi.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria matamshi ya Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki aliyeelezea uwezekano wa malalamiko ya hivi karibuni ya wanachi wa Iraq kutokea pia nchini Iran na kuweko njama nyuma yake na kusema kuwa, matamshi ya Erdogan kwa hakika kwa namna fulani ni tahadhari nzuri ambayo imetolewa kwa wakati wake kwani nchi za eneo zinapaswa kuwa macho na makini.
Sayyid Abbas Mousavi ameashiria msimamo mkali wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa baada ya Iran kuanza kutekeleza hatua ya nne ya kupunguza uwajibikaji wake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, msimamo wa Macron mtu unaweza kuudiriki.
Ameongeza kuwa, madola ya Ulaya yametambua kuwa, Tehran haina mzaha hata kidogo katika misimamo yake na katika upande mwingine madola hayo yameshindwa kutoa majibu kutokana na udhaifu wao.
.........
340